Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chama cha msalaba mwekundu limethibitisha kuachiliwa kwa mfanyakazi wake Darfur:

Chama cha msalaba mwekundu limethibitisha kuachiliwa kwa mfanyakazi wake Darfur:

Kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu ICRC imethibitisha kwamba mmoja wa wafanyakazi wake aliyetekwa mgharibi mwa Darfur mwaka jana ameachiliwa huru.

Kwa mujibu wa shirika hilo Gauthier Lefevre ameachiliwa leo karibu na mji wa Geneina ambao ni makao makuu ya jimbo la Darfur Magharibi baada ya kushikiliwa kwa siku 147.

Bwana Lefevre alionekana ni mchovu sana lakini yuko katika afya njema. ICRC inasema imefurahi kwa kuachiliwa kwa mtu huyo ambayo hivi karibuni atakwenda kujiunga na familia na marafiki zake ambao kwa miezi mitano walikuwa katika hali ngumu ya kutojua hatma yake.

ICRC ilianza kufanya kazi nchini Sudan mwaka 1978. Na tangu mwaka 2004 imekuwa ikisaidia sana watu wa Darfur wanaoathirika na vita vinavyoendelea. ICRC inasema lengo lake ni kuhakikisha watu wanaoathirika na vita wanalindwa kwa kupata misaada ya dharura kutokana na sheria za kimataifa, ikiwemo chakula, matibabu na mingineyo.