Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA inayadadisi maelezo ya sheria itkayompa udhibiti wa tume ya malalamiko ya uchaguzi rais Karzai

UNAMA inayadadisi maelezo ya sheria itkayompa udhibiti wa tume ya malalamiko ya uchaguzi rais Karzai

Mpango wa usaidizi wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA, hivi sasa unayapitia kwa undani maelezo ya mswaada wa sheria uliopendekezwa na Rais wa nchini hiyo Harmid Karzai ,ambao utampa mamlaka ya kudhibiti tume ya malalamiko ya uchaguzi.

Mswaad huo tayari umeanza kuzusha maswali mengi juu ya uhalali wake na kama itakuwa ikitenda haki dhidi ya malalamiko ya uchaguzi.

Akijibu maswali kuhusu mswaada huo msemaji wa UNAMA Dan Mc Norton amesema ni bila shaka wanataka kuona uhalali na usawa katika uchaguzi wa bunge utakofanyika mwaka huu na wanatumaini katiba itazingatiwa.