Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakili ateuliwa kuwa mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya uhalifu Sierra Leone

Wakili ateuliwa kuwa mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya uhalifu Sierra Leone

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua wanasheria wa Marekani Brenda Joyce Hollis ambaye alikuwa akiongoza upande wa mashitaka dhidi ya kesi ya Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor, kuwa mwendesha mashitaka mpya wa mahakama ya uhalifu ya Sierra Leone inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Mahakama hiyo inaendesha na kuhumu kesi za uhalifu uliotendeka katika muongo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone. Tangu mwaka 2007 Bi Hollis amekuwa akifanya kazi katika mahakama maalumu ya uhalifu ya Sierra Leone kama mwanasheria wa masuala ya kesi kwenye ofisi ya mwendesha mashitaka.

Bi Hollis pia alisaidia waathirika wa uhalifu wa kimataifa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Colombia kuwasilisha maombi ya uchunguzi kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC The Hague . Na pia alifanya kazi na mahaka ya kimataifa ya uhalifu uliotendeka Yugoslavia.