Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpatanishi wa mgogoro wa kisiasa wa Ivory Coast anakwenda Abidjan

Mpatanishi wa mgogoro wa kisiasa wa Ivory Coast anakwenda Abidjan

Mpatanishi wa mgogoro wa kisiasa wa Ivory Coast, Rais wa Blaise Compaore wa Burkina Faso leo amekwenda mjini Abijan kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa serikali na upande wa upinzani ili kumaliza mgogoro huo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea hofu yake juu ya mvutano huo wa Ivory Coast na amezitaka pande husika kumaliza tofauti zao kwa njia ya mazungumzo. Amewataka pia katika mazungumzo yao kuzingatia makubaliano ya kisiasa ya Ouagadougou.