Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM asema mwaka huu ni muhimu kwa Sudan

Mwakilishi wa UM asema mwaka huu ni muhimu kwa Sudan

Mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeondoka nchini Sudan Ashraf Qazi anasema mwaka huu wa 2010 ni mwaka muhimu saana kwa Sudan.

Katika hafla ya kumuaga mwishoni mwa wiki mjini Khartoum bwana Qazi amepongeza nchi hiyo kwa hatua iliyopiga katika mchakato wa uchaguzi na utekelezaji wa mkataba wa amani wa mwaka 2005 ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe baiana ya Kaskazini na Kusini mwa Sudan.

Hata hivyo amesema bado kuna changamoto nyingi zinazoikabili nchi hiyo na ameonya ,dhidi ya mabadiliko ambayo yanaweza kubadili hali nzuri ya sasa. Bwana Qazi ambaye anaondoka Sudan kwa sababu binafsi na za kifamilia nafasi yake itachukuliwa na Haile Menkerios.