Hofu yatanda dhidi ya hatma ya watoto wa Haiti

Hofu yatanda dhidi ya hatma ya watoto wa Haiti

Kundi la wataalamu wa masuala ya haki za binadamu limeonya juu ya ongezeko la athari zitakazowasibu watoto wa Haiti, wakiwemo yatima.

Athari hizo ni pamoja ya kutekwa, kuuzwa au kusafirishwa nje bila ridhaa yao. Hatua hii inatokana na usalama mdogo nchini humo kufuatia tetemeko la ardhi lililoikumba Haiti hivi karibuni.

Wataalamu hao wanaoongozwa na baraza la haki za binadamu , kuangalia masuala ya utumwa, uuzaji wa watoto, usafirishaji wa watoto kinyume cha sheria, na ukatili dhidi ya watoto, wamesisitiza kuwa suala la kuwalinda watoto lazima lipewe umuhimu mkubwa katika shughuli za misaada nchini Haiti.

Kamishana mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu, kamati ya haki za watoto na wataalamu binafsi nchini humo pia wamehimiza kuwalinda watoto hasa kuokana na magenge ya wahalifu walitoroka jela baada ya jela hizo kuharibiwa na tetemeko la ardhi.