Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idara ya kupambana na uhalifu ya UM kuazisha chuo cha polisi Guinea-Bissau

Idara ya kupambana na uhalifu ya UM kuazisha chuo cha polisi Guinea-Bissau

Idara ya kupambana na uhalifu ya Umoja wa mataifa itasaidia juhudu za kuikarabati Guinea-Bissau kua mahala penya usalama na utulivu kwa kujenga chuo cha mafunzo kwa ajili ya vikosi vya usalama vya taifa hilo la Afrika Magharibi.

Kufuatana na afisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa ya kuelvya na uhalifu UNODC, Guinea-Bissau ambayo ilishuhudia vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe mwishoni mwa miaka ya 1990, imekua kituo kipya cha biashara ya magendo ya madawa ya kulevya hasa cocaine kutokea Amerika ya kusini kuelekea Ulaya. UNODC imeeleza kwamba kuna haja ya dharura kukabiliana na uhalifu wa magengi, kwa mtizamo wa kufanya mageuzi ya usalama na kuimarisha utawala wa mahakama na utawala wa sheria katika nchi hiyo. Afisi ya kikanda ya UNODC kwa ajili ya Brazil na Amerika ya Kuisni imesimamia makubaliano kati ya Brazil na Guinea-Bissau kuunda chuo cha polisi ambacho kitaimarisha vikosi vya usalama vya Guinea pamoja na kuisaidia serekali kutekeleza mpango wake wa kitaifa kupambana na madawa ya kulevya na uhalifu. Mradi huo wa miaka mitatu utakao gharimu dola milioni 3 kutoka idara ya ushirikiano ya Brazil itasimamiwa na UNODC na idara ya polisi ya Brazil kutoa mafunzo kwa maafisa wa usalama wa Guinea.