Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ametoa wito wa kustahmiliana huko Nigeria

Ban ametoa wito wa kustahmiliana huko Nigeria

Katibu mkuu wa UM Ban Ki-moon alitoa wito siku ya Alhamisi kwa watu kustahmiliana kufuatia mapigano ya kidini ya siku nne yaliyosababisha maafa ya karibu watu 200 katika mji wa Jose eneo la kati nchini Nigeria.

Alitoa wito pia kwa wote wanaohusika kutafuta suluhisho kwa njia ya amani kwa tofauti zao za kidini na matatizo mengine nchini humo. Taarifa iliyotolewa na msemaji wake inaeleza kwamba Bw Ban anatoa wito hasa kwa viongozi wote wa kisiasa na kidini huko Nigeria kufanya kazi pamoja kutanzua matatizo msingi yanayosababisha kuzuka mara kwa mara ghasia za kidini nchini humo. Alitilia maanani juhudi za serekali kujaribu kutafuta suluhisho la kudumu kwa mzozo huo wa Jose, na kuhimiza kuwepo na kila juhudi za kurudisha utulivu na kuepusha kuzorota tena kwa hali huko.