Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unataraji uchumi dunia kufufua kidogo

UM unataraji uchumi dunia kufufua kidogo

Katika ripoti yake kuhusiana na hali ya uchumi duniani na matarajiyo yake UM umeeleza kwamba kuanzia robo ya pili ya mwaka jana, hali ya uchumi duniani imekua ikianza kurudi kua ya kawaida.

Kinachoonekana ni kufufuka kwa masoko ya hisa duniani, pamoja na biashara ya kimataifa na uzalishaji viwandani. Ripoti hata hivyo inaonya kwamba kufufuka huko hautokei kwa usawa na hali ya ukuwaji wa kudumu ingali ni tete. Idadi ya ukosefu ajira inatarajiwa kubaki juu kwa 2010. Alfredo Calcagno mtalamu wa uchumi katika Idara ya biashara na maendeleo ya UM UNCTAD anasema

"Utabiri ulowasilishwa kwenye ripoti hii aonesha ukuwaji wa asili mia 2.4 kwa uchumi wa dunia kwa mwaka 2010, kukiwepo na ukuwaji mdogo sana katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea na ni ukuwaji ambao unategemea zaidi mipango ya fedha zilizotoilewa ili kufufua uchumi."

Ripoti ya UM inapendeleza kwamba mipango ya kufufua uchumi inabidi kuendelea hadi kumekuwepo na ishara za wazi zaidi za kuimarika kwa ukosefu wa ajira. Matiafa yanayoendelea hasa yale ya Asia yanatazamiwa kuwa na ukuwaji mkubwa wa asili mia 5.3 kwa mwaka huu.