Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unaitaka serekali ya Uganda kuondowa mswada dhidi ya watu wa jinsia moja wanaopendana

UM unaitaka serekali ya Uganda kuondowa mswada dhidi ya watu wa jinsia moja wanaopendana

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu Navi Pillay aliihimiza serekali ya Uganda siku ya Ijumaa kutupilia mbali mswada wa sheria kuhusiana na watu wa jinsia moja wanaopendana, ambao unatarajiwa kufikishwa bungeni mwishoni mwa mwezi Januari.

Alisema mswada huo utaisababisha nchi hiyo kujikuta katika mvutano wa moja kwa moja na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu vyenye lengo la kuzuia ubaguzi. Bi Pillay alipongeza taarifa za hivi karibuni za rais na mawaziri wake zikidokeza huwenda wakaingilia kati kuzuia mswada huo ulowasilishwa kibinafsi na mbunge ili kupitishwa kua sheria. Hata hivyo waziri wa habari wa Uganda Agrey Awori amesema kufuatana na katiba ya Uganda, tabia ya watu wa jinsia moja kupendana imepigwa marufuku, hivyo mswada huo unahusiana na utekelezaji wa sheria hiyo.

AWORI: mwanzo iko katika katiba yetu kwamba watu wa ...

Bw Awori alisema kufuatana na katiba na misingi ya kidemokrasia kwa wakati huu rais hana uwezo wa kuuondowa mswada huo kwa vile sheria za nchi zinalipatia bunge uhuru wa kuchukua uwamuzi bila ya mamlaka ya rais kuingilia kati.

AWORI: hawezi kuiondowa kwa sababi si haki yake kwa wakati wa sasa....

Mswada huo wa sheria dhidi ya watu wajinsia moja wanaopendana ulowasilishwa na mbunge mmoja na kuungwa mkono na wabunge wengi, unapiga marufuku uhusiano wa aina yeyote ya mapenzi ya watu wa jinsia moja, pamoja na kuendeleza au kuhamasisha kua maisha yanayokubalika au ya haki katika tasisi zote za umma.

Bi Pillay anasema mswada unapendekeza adhabu kali za kikatili kwa watu watakao tuhumiwa kua na uhusiano au mapenzi ya jinsia moja, yaani kifungo cha maisha jela au katika baadhi ya matukio hukumu ya kifo. Na hivyo anasema ni ajabu sana kupata sheria kama hiyo inapendekezwa karibu miaka 60 baada ya kuidhinishwa kwa mkataba wa kimataifa wa Haki za Binadamu, pamoja na sheria na viwango mbali mbali vya kimataifa kueleza bayana kwamba ubaguzi haikubaliki kamwe.

Licha ya kishinikizo cha kimataifa Bw Awori anasema serekali imeshauriwa kusubiri hadi mswada unapita bungeni ndipo uwamuzi wa mwisho utachukuliwa.

AWORI: Mswada huo kwanza serekali imesema tusubiri

Kamishna mkuu wa Haki za Binadamu anasema mswada huo bila shaka unakiuka viwango vya kimataifa vya haki za binadamu kwa vile ni wa ubaguzi uliyo bayana, akiongeza kusema ikiwa mswada utapita utakua na athari mbaya sana kwa nafasi kadhaa katika haki za binadamu wanaopatiwa watu wa jinsia moja wanaopendana.

Bi Pillay alisema angelipenda kuikumbusha serekali ya Uganda kwamba chini ya sheria ya Kimataifa ya Haki za Binadamu, kama nchi iliyoidhinisha mkataba huo wa kimataifa inawajibu wake wa kulinda sheria hizo na kawaida imekua na ushirikiano mzuri na utaratibu mbali mbali za kimataifa za haki za binadamu. Lakini mswada huo utaweza kuharibu vibaya sana sifa zake katika jukwaa la kimatiafa.