Skip to main content

Eide ameonya kuendelea kwa mtafaruku wa kisiasa baada ya bunge la Afghanistan kulikataa Baraza la Mawaziri lililoteuliwa

Eide ameonya kuendelea kwa mtafaruku wa kisiasa baada ya bunge la Afghanistan kulikataa Baraza la Mawaziri lililoteuliwa

Kukataliwa na wabunge sehemu kubwa ya baraza hilo jipya la Rais Hamid Karzai ni pigo la kisiasa kwa nchi hiyo, amesema Mjumbe Maalumu wa KM nchini Afghanistan Kai Eide .

Bwana Eide amesema hali hiyo itachagiza kuendelea kutofanya kazi ipasavyo serikali hiyo na kwamba ni hali inayotia hofu kwa nchi ambayo inakabiliwa na changamoto nyingi. Kwa mujibu wa duru mbalimbali, Eide amesema, "Afghanistan haijawa na utawala muri tangu majira ya joto mwaka jana na bunge linachochea hali hii.."