Wahamiaji wa mataifa jirani katika Sudan wanahitajia huduma za msingi haraka kumudu maisha, imeonya UNHCR

30 Disemba 2009

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeeleza UM kwamba liliwajibika kushughulikia kihali jumla ya wahamiaji 66,000 waliomiminikia kwenye kambi za wahamiaji ziliopo Sudan mashariki, kutokea Eritrea, Ethiopia na Usomali.

 UNHCR ilisema hali ya wahamiaji muhitaji wa mataifa ya Pembe ya Afrika, haitambulikani sana na jamii ya kimataifa kama ule mzozo wa Darfur. Ripoti ya UNHCR ilisema wahamiaji hawa wamenyimwa huduma za kimsingi, na watoto wao wamekosa uwezo wa kupata elimu, na wote huishi kwenye mazingira magumu kabisa. George Okoth-Okobo, Mkurugenzi wa Idara juu ya Afrika katika Shirika la UNHCR alinakiliwa akisema "umasikini uliovuka mipaka, ikichanganyika na ukame wa muda mrefu kwenye kambi za wahamiaji, ukosefu wa huduma za afya na elimu, na ukosefu mkubwa wa ajira pamoja na ardhi ilioharibika na maeneo ya malisho ya wanyama yaliokauka" ni mambo yenye kuhatarisha maisha ya wahamiaji wa Eritrea, Ethiopia na Usomali waliopo Sudan Mashariki, umma ambao unahitajia kufadhiliwa kidharura misaada ya kimataifa na kuwawezesha kumudu maisha ya kawaida.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter