Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lazingatia hali katika Usomali, na kazi za Mahakama za ICTY na ICTR

Baraza la Usalama lazingatia hali katika Usomali, na kazi za Mahakama za ICTY na ICTR

Alasiri Baraza la Usalama linatarajiwa kukutana kujadilia maendeleo ya karibuni katika Usomali.

Asubuhi Baraza la Usalama lilikutana kusikiliza ripoti mpya za Maraisi na waendesha mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Vita kwa Yugoslavia ya Zamani (ICTY) na Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki kwa Rwanda (ICTR). Maofisa wa mahakama hizi mbili walielezea taratibu juu ya namna watakavyokamilisha shughuli na kazi za taasisi hizi za kimataifa katika siku za baadaye.