Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na mashirika ya misaada ya kiutu yaomba yafadhiliwe $689 kuisaidia Usomali kwa 2010

UM na mashirika ya misaada ya kiutu yaomba yafadhiliwe $689 kuisaidia Usomali kwa 2010

Vile vile kuhusu hali katika Usomali, kutokea Nairobi, kumeanzishwa hii leo kampeni maalumu ya kuchangisha misaada ya kiutu inayokaribia dola milioni 700, fedha zinazohitajika kufadhilia miradi 174 katika 2010,

mipango inayosimamiwa na mashirika 14 ya UM pamoja na mashirika yasio ya kiserikali ya kizalendo na kimataifa 57 ili kukidhi bora mahitaji ya dharura ya waathirika wa misukosuko ya kimaisha katika Usomali. Misaada itatumiwa kwenye huduma za kunusuru maisha; katika kuongeza na kulinda mali zinazoambatana na maendeleo ya kiuchumi na jamii, na hifadhi ya mazingira; na kwenye huduma za kimsingi kwa raia dhaifu kimaisha, hasa wale wanawake na vijana ambao pia huhitajia hifadhi imara kwenye mazingira yaliojaa wasiwasi na uhasama. Kampeni ya kuchangisha misaada ya kihali kwa Usomali iliongozwa na Mark Bowden, Mratibu Mkaazi wa UM juu ya Misaada ya Kiutu kwa Usomali aliopo Nairobi.