Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulio la kujitoa mhanga Usomali kulaaniwa na mashirika ya kimataifa, ikijumlisha UM

Shambulio la kujitoa mhanga Usomali kulaaniwa na mashirika ya kimataifa, ikijumlisha UM

Hii leo, kutoka mjini Nairobi, Kenya mashirika kadha yenye kujumuisha jumuiya ya kimataifa yametoa taarifa ya pamoja, iliolaani kwa kauli kali, tukio la bomu la kujitolea mhanga liliofanyika Alkhamisi kwenye mji mkuu wa Usomali wa Mogadishu ambapo maofisa kadha wa Serikali ya Mpito waliuawa pamoja na wanafunzi, waandishi habari na raia wengine.