Hapa na pale

13 Novemba 2009

Kwenye mkesha wa Mkutano Mkuu juu ya Udhibiti Bora wa Akiba ya Chakula Duniani, utakaofanyika wiki ijayo kwenye mjini Roma, Utaliana, kulitolewa ilani maalumu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) yenye kuuhimiza umma wa kimataifa kufanyisha mgomo wa siku moja dhidi ya tatizo la njaa sugu iliokabili mamilioni ya watu kwenye sayari ya dunia yetu. Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Jacques Diouf amependekeza kwamba kila mwanadamu mwenye hisia halisi juu ya mateso ya njaa sugu wanaopata watu bilioni moja ulimwenguni, wajaribu kufunga ama katika Ijumamosi au Ijumapili ijayo. Alisema yeye binafsi ataanza kufunga, kwa muda wa saa 24, kuanzia Ijumamosi asubuhi ya tarehe 14 Novemba 2009.

Sha Zukang, Naibu KM juu ya Masuala ya Uchumi na Jamii yupo Vienna, Austria leo hii akihudhuria kongamano maalumu, la Hadhi ya Juu, litakalosailia mada kuhusu "Ushirikiano Ulio Wazi na Wenye Uwajibikaji Kuhudumia Maendeleo: Kwa mwelekeo wenye mfumo utakaojumlisha kila mtu". Kongamano hii, ilisema taarifa ya UM, unahusiana na matayarisho ya ‘Mkutano wa 2010 wa ECOSOC juu ya Ushirikiano wa Huduma za Maendeleo". Sha Zukang, kwenye risala yake ya ufunguzi, alisema anaamini kongamano yao imebarikiwa uwezo wa aina ya pekee, katika kutathminia namna wadau wanaoshughulikia huduma za maendeleo wanavyotekeleza ahadi zao; pamoja na kuwa na fursa ya kuzingatia kama ushirikiano kama huo unafaa kuendelezwa ili kuimarisha malengo ya maendeleo yalioafikiwa kimataifa kwa mafanikio.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter