Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suluhu hakika yahitajika kudhibiti upungufu wa maji unaosababishwa na hali ya hewa ya kigeugeu

Suluhu hakika yahitajika kudhibiti upungufu wa maji unaosababishwa na hali ya hewa ya kigeugeu

Wiki hii tunajadilia umuhimu wa kuzingatia, kwa kina, mchango wa maji safi na salama, katika udhibiti bora wa mabadiliko ya hali ya hewa.

Shinikizo zinazoletwa na mifumko ya idadi ya watu duniani, ikichanganyika na athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwenye akiba ya maji safi ya matumizi, ni masuala yanayohitajia suluhu ya dharura, kwa sababu inakhofiwa tutakapofikia katikati ya karne ya 21, tutalazimika kulisha idadi kubwa ya watu duniani, katika mazingira ya ulimwengu ambayo, vile vile, uatavamiwa na upungufu wa hali ya juu wa akiba ya maji. Kwenye majadiliano ya Kamati ya Baraza Kuu juu ya Masuala ya Fedha na Uchumi, au Kamati ya Pili, wataalamu wawili kutoka UM na vilevile kutoka taasisi ya kimataifa inayoshughulikia matatizo ya maji, walizingatia na kutafakaria fungamano ziliopo baina ya mabadiliko ya hali ya hewa na namna yatakavyoathiri mifumko ya idadi ya watu, kwa siku za baadaye. Matatizo haya yaichanganyika na upungufu wa maji safi na salama unaoashiriwa kujiri katika 2050 na mambo yanayotakiwa kupatiwa suluhu ya mapema kabla hayajatota na kuwa janga la maangamizi kwa mazingira na umma, halkadhalika.

Sikiliza kipindi kamili kwenye idhaa ya mtandao.