Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uokozi wa awali wa watoto waliotoroshwa Sudan kusini kupongezwa na UM

Uokozi wa awali wa watoto waliotoroshwa Sudan kusini kupongezwa na UM

UM umepongeza kuokolewa watoto 28 waliotekwa nyara siku za nyuma katika Jimbo la Jonglei, Sudan Kusini.

Lise Grande, Kaimu Mkazi wa UM na Mratibu wa Misaada ya Dharura katika Sudan alitoa mwito uliowataka maofisa husika wa utawala kuhakikisha watoto wote walionyakuliwa kiharamu na kuwekwa vizuizini, waachiwe haraka, na ile "tabia ya kuwatorosha watoto ikomeshwe, halan, katika Sudan kusini na makundi yote husika na jinai hii." Watoto 28 wa umri wa baina ya miaka 2 na 14, waliachiwa mnamo tarehe 22 Oktoba, kufuatia uamuzi wa Kamishna wa wilaya ya Pibor, ambaye aliahidi kusitisha janga la kuiba watoto katika jimbo la Jonglei. Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kwamba kuanzia mwanzo wa 2009 maelfu ya watoto wadogo waling'olewa makazi, kwa sababu ya mashambulio ya kundi la waasi wa Uganda linalojidai kuwa ni Jeshi la Upinzani la Bwana Mngu (LRA), yaliofanyika kwenye sehemu za Equatoria ya Kati na Magharibi, wakati mapigano ya kikabila katika majimbo ya Jonglei, Lakes na Warrap nayo vile vile yanaaminika yalisababisha vifo na watoto kadha kutoroshwa. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani Sudan Kuisni (UNMIS), watoto walioachiwa sasa hivi wanajumlisha raia wa Ethiopia tisa kutokea jimbo la Gambella, na watoto wanane, wakazi wa majimbo ya Equatoria ya Kati na Mashariki, Sudan kusini.