Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mgombea uraisi Afghanistan alijitoa kwenye duru ya pili ya uchaguzi ambayo anasema hairidhishi kisheria

Mgombea uraisi Afghanistan alijitoa kwenye duru ya pili ya uchaguzi ambayo anasema hairidhishi kisheria

Mgombea uraisi wa Afghanistan, Abdullah Abdullah, aliripotiwa Ijumapili kujitoa kwenye duru ya pili ya uchaguzi ilioandaliwa kufanyika tarehe 07 Novemba.

 Moja ya sababu ilizomfanya Abdullah kutoshiriki kwenye duru ya pili ya uchaguzi wa uraisi alisema ni kwamba haamaini utaribu uliopo hivi sasa, umerekibishwa kwa kiwango kitakachohakikisha wapiga kura watahifadhiwa na udanganyifu, kama ule uliotendeka kwenye uchaguzi wa duru ya kwanza ya uchaguzi, mnamo tarehe 20 Agosti mwaka huu. Lakini juu ya uamuzi huo, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Afghanistan, Kai Eide alinakiliwa akisema ana matumaini uchaguzi wa wiki ujao "utakamilishwa kwa kufuata sheria na kwa wakati." Alisema anaamini uamuzi wa Abdullah ulichukuliwa "baada ya kutafakaria kwa kipindi kirefu juu yahuduma za duru ya pili ya uchaguzi wa uraisi", katika Afghanistan, na anatumai mapendekezo ya Abdullah Abdulla ya kurekibisha huduma za uchaguzi yatazingatiwa kwenye ajenda ya masuala ya kisiasa katika Afghanistan kwa siku za baadaye.