Skip to main content

FAO imeripoti kuwa uwekezaji kwenye utafiti wa kilimo ni muhimu kwa maendeleo

FAO imeripoti kuwa uwekezaji kwenye utafiti wa kilimo ni muhimu kwa maendeleo

Ripoti iliochapishwa hii leo na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) imeeleza Mataifa Wanachama yatahitajia kuwekeza, kwa kiwango kikubwa zaidi, kwenye shughuli za utafiti ambao matokeo yake yatayawezesha mataifa, hasa zile nchi masikini, kutumia teknolojia mpya ya ukulima na kwenye matumizi ya mazao makuu tofauti yatakayosaidia kuzalisha mavuno kwa wingi zaidi.

Ripoti hii ni miongoni mwa taarifa zinazotayarishwa kabla ya kufanyika kikao cha hadhi ya juu cha wataalamu, kwenye mji wa Roma, yalipo Makao Makuu ya FAO, kuanzia tarehe 12 mpaka 13 Oktoba mwaka huu. Mkutano unatazamiwa kuzingatia utaratibu unaofaa kutekelezwa na Mataifa Wanachama utakaohakikisha itakapofika 2050 walimwengu watakuwa na akiba maridhawa ya chakula, itakayokidhi vyema mahitaji ya umma wa kimataifa kote ulimwenguni.