Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanadamu anaweza kuambukiza mnyama A/H1N1, inasema WHO

Mwanadamu anaweza kuambukiza mnyama A/H1N1, inasema WHO

Imetangazwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ya kwamba kuna uwezekano kwa wanadamu, mara kwa mara, kuwaambukiza wanyama wa mifugo, kama nguruwe, kuku na mabata yale maradhi ya homa ya mafua ya aina ya A/H1N1.

Gregory Hartl, msemaji wa WHO, alipokutana na waandishi habari mjini Geneva, Ijumanne asubuhi, alithibitisha ugunduzi huo. Alihadharisha kwenye taarifa yake ya kwamba ni muhimu kwa wahudumia afya kufuatilia mapema maambukizi kama haya ya maradhi ya kutoka mwanadamu dhidi ya wanyama, ili kudhibiti virusi vya maradhi visije vikaenea zaidi miongoni mwa makundi ya wanyama wa mifugo. Aliongeza kusema ya kuwa hadi hivi sasa hakuna taarifa zozote zilizopokelewa na WHO zenye kuonyesha maambukizi ya homa ya H1N1 ya kutoka mwanadamu na kumwingia mnyama yalisambaa nje ya makundi ya wanyama walioambukizwa nayo hapo mwanzo.