Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano ya kikabila Kenya yamesababisha maelfu ya wakuria kung'olewa makazi

Mapigano ya kikabila Kenya yamesababisha maelfu ya wakuria kung'olewa makazi

Shirika la UM juu ya Huduma za Dharura (OCHA) limetangaza kupamba hali ya wasiwasi mkuu kwenye wilaya ya Kenya ya Kuria Mashariki, karibu na mpaka na Tanzania, ambapo majuzi watu 6,000 waling\'olewa makazi kwa sababu ya mapigano yaliozuka miongoni mwa jamii ya makabila ya Kuria.