Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM amehuzunishwa sana na uvamizi wa kunajisi kimabavu wanawake wafungwa katika JKK

KM amehuzunishwa sana na uvamizi wa kunajisi kimabavu wanawake wafungwa katika JKK

KM Ban Ki-moon ametangaza kuhuzunishwa sana na ripoti alizopokea karibuni, kuhusu tukio la uvamizi na vitendo vya kunajisi kimabavu, wafungwa wanawake 20 waliojaribu majuzi kukimbia kutoka gereza kuu la Goma, liliopo katika eneo la mashariki ndani ya JKK.

Tukio hili liliripotiwa kusababisha vifo na majeruhi kadha. Ofisi ya msemaji wa KM ilimnukuu Ban Ki-moon akisema tukio la gereza ya Goma, linadhihirisha wazi "mfano katili kuhusu mazingira halisi yaliojiri ya magereza, na viwango vya ukabaji na udhalilishaji wa kijinsiya ulioliambukiza JKK." KM aliisihi Serikali ya JKK kuwashika na kuwafikisha mahakamani kukabili haki wale wote waliofanya makosa ya kuwanajisi kimabavu wanawake wafungwa, na kujaribu kufufua zile jitihadi za kukomesha tabia karaha ya wakosaji wanaoendeleza ukatili wa kunajisi wanawake kimabavu bila ya kukhofu adhabu.