Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makampuni ya madawa yaombwa na KM kushirikiana kimataifa kudhibiti vyema homa ya A(H1N1)

Makampuni ya madawa yaombwa na KM kushirikiana kimataifa kudhibiti vyema homa ya A(H1N1)

KM Ban Ki-moon kwenye risala yake mbele ya kikao cha 62 cha Baraza Kuu la Afya Duniani, kilichofunguliwa rasmi mapema wiki hii mjini Geneva, aliyahimiza makampuni yenye kutengeneza madawa kushirikiana na serikali wanachama katika kutafuta suluhu ya dharura, ili kuulinda ulimwengu na maambukizi hatari ya mripuko wa karibuni wa maradhi ya homa ya mafua ya A(H1N1).

Alikumbusha ya kwamba virusi vya H1N,1 kwa sasa, vimeshagunduliwa kudhuru raia katika nchi 40, ikimaanisha ulazima wa viongozi wa sekta za binafsi na zile za umma kushirikiana, kidharura, ili kudhibiti pamoja haraka tatizo la maambukizi ya maradhi haya, ambayo usambazaji wake umebainisha fungamano zilizodhihiri kihakika baina ya mataifa katika ulimwengu wa sasa.