Mashitaka mapya dhidi ya Aung San Suu Kyi yalaumiwa na Navi Pillay

18 Mei 2009

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay, Ijumaa alishtumu taarifa zilizoonyesha kwamba wenye mamlaka Myanmar walimfungulia mashitaka mapya mpinzani, Aung San Suu Kyi. Aliwasihi kufuta msururu wa mashitaka ambayo yanafungamana na tukio nje ya uwezo wa Aung San Suu Kyi.

Pillay aliwasihi wenye madaraka Myanmar kumwachia, haraka, Aung San Suu Kyi kutoka uzuizi unaoendelea, kitendo ambacho, alisisitiza, hutengua sheria za kitaifa za Myanmar, yenyewe, halkadhalika, na pia huvunja misingi ya "sheria ya kimataifa ya usikilizaji wa mashitaka na haki ya kujitetetea" ya mtuhumiwa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter