Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa Wanachama yanahimizwa kuharakisha utekelezaji wa ahadi za Brussels kuhudumia amani Usomali

Mataifa Wanachama yanahimizwa kuharakisha utekelezaji wa ahadi za Brussels kuhudumia amani Usomali

Ahmedou Ould Abdalah, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali ameripotiwa kutoa taarifa inayohimiza nchi wanachama zilizohudhuria Mkutano wa Brussels juu ya Usomali, uliofanyika wiki iliopita ambapo kuliahidiwa kuchangisha msaada wa dola milioni 213 ziada, kukamilisha ahadi zao haraka iwezekanavyo, ili kuviwezesha vikosi vya ulinzi amani kuimarisha utulivu nchini Usomali.