Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama linazingatia tena operesheni za UNAMID

Baraza la Usalama linazingatia tena operesheni za UNAMID

Baraza la Usalama asubuhi limezingatia ripoti ya KM kuhusu maendeleo kwenye operesheni za kulinda amani Darfur za vikosi vya mchanganyiko vya UM na UA, yaani vikosi vya UNAMID.

Mkuu wa UNAMID, Rodolpho Adada alipohutubia wajumbe wa Baraza alisema huduma za kurudisha utulivu na amani kwenye eneo hili zimezorota kwa sasa hivi, na mchango maridhawa wa kimataifa utahitajika haraka kuisaidia UNAMID kuweza kudhibiti vyema shughuli zake kieneo.