Skip to main content

KM ametangaza sera mpya juu ya uhusiano wa kimataifa

KM ametangaza sera mpya juu ya uhusiano wa kimataifa

Kwenye hotuba aliyoiwakilisha mbele ya wajumbe waliohudhuria warsha maalumu, leo asubuhi, katika Chuo Kikuu cha Princeton, kilichopo Jimbo la New Jersey, Marekani KM Ban Ki-moon alibainisha mtazamo wa sera mpya ya kimataifa juu ya uhusiano wa pande nyingi, miongoni mwa nchi wanachama.

KM alitarajia uhusiano wa siku za usoni utajumlisha ushirikiano utaolenga zaidi kwenye shughuli za kuimarisha utulivu unaosarifika wa huduma za uchumi na fedha katika soko la kimataifa, ambapo pia kutahitajika msukumo mkubwa kwenye huduma za kukomesha ufukara na umasikini, na katika kurudisha utulivu wa amani, pamoja na udhibiti wa mabadiliko ya hali ya hewa, ukomeshaji wa vitendo vya ugaidi pamoja na kupunguza ueneaji wa silaha za kinyuklia ulimwenguni, na kuhakikisha pia ya kwamba UM huwa inapatiwa madaraka zaidi ya kuiwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu.