Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakaguzi wa IAEA wapigwa marufuku Korea ya Kaskazini

Wakaguzi wa IAEA wapigwa marufuku Korea ya Kaskazini

Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) limeripoti kwamba wakaguzi wa UM waliohusika na uchunguzi wa shughuli za kiwanda cha nishati ya nyuklia, kiliopo kwenye mji wa Yongbyon, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea (Korea Kaskazini) wamelazimika kuondoka nchini Alkhamisi ya leo.

Wakaguzi hawa walihama Korea Kaskazini baada ya kuondosha vifaa vya IAEA pamoja na kamera za uchunguzi kutoka kile kiwanda cha Yongbyon, kuridhia ile amri ya Serikali ya Korea Kaskazini ilioarifiwa IAEA, mnamo Ijumanne ya tarehe 14 Aprili, ya kwamba watasitisha, halan, ushirikiano wote na taasisi hii ya UM.