KM amelaani shambulio la kigaidi huko Lebanon

24 Machi 2009

KM Ban Ki-moon amelaani shambulio la kigaidi jana lililosababisha kifo cha Kamal Medhat, naibu mkuu wa chama cha ukombozi wa Palestina PLO huko Lebanon, na baadhi ya walinzi wake.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake inaeleza kwamba ana matumiani wahalifu wa kitendo hicho watafikishwa mahakamani haraka. Akisema hatua kama hizi haizjabidi kuruhusiwa kuhatarisha hali ya utulivu inayoendelea kwa wakati huu huko Lebanon. Kufuatana na ripoti za vyombo vya habari, bomu lililotegwa kando ya barabara liliripuka wakati mlolongo wa magari ya Bw Medhat yalipokua yanaondoka kutoka kambi ya wakimbizi wa ki-Palestina huko Lebanon ya Kusini.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter