Rais wa Madagascar astahafu na kukabidhi majeshi madaraka
KM Ban Ki-moon amezihimiza pande zote huko Madagascar kuhakikisha utulivu na mpito makini wa kidemokrasiakufuatia kujiuzulu kwa rais Marc Ravalomanana.
Taarifa iliyotolewa na msemaji wake inaeleza kwamba njia ya amani inaweza kupatikana kutokana na utaratibu wa mtipo utakaofikiwa kwa maridhiano na kuungwa mkono na wengi. Rais Marc Ravalomanana wa Madagascar amejiuzulu Ijumanne na kukabidhi madaraka kwa jeshi la taifa kufuatia mvutano na upinzani. Rais alitangaza kwenye redio ya taifa kwamba anaacha madaraka na kukabidhi mamlaka kwa kundi la viongozi wa kijeshi wanaogozwa na Admirali wa jeshi la majini Hyppolite Ramaroson. Meya wa zamani wa mji mkuu Andry Rajoelina aliyekua akivutana na rais Ravalomanana na kuongoza malalamiko ya wananchi kwa wiki kadhaa hakusema lolote juu ya tangazo hilo. Bw Rajoelina hata hivyo alishangiriwa na wafuasi wake na wanajeshi waloasi Jumanne alipoingia katika ikulu ya rais iliyokua tupu katika mji mkuu wa Antananarivo. Viongozi wa kidini walianda ibada kuadhimisha tukiyo hilo.