Kamishna wa Haki za Binadamu anatoa ripoti juu ya kazi zake DRC
Naibu kamishna wa Haki za Binadam alitoa ripoti ya kamishna mkuu juu ya hali ya haki za binadam na kazi za afisi hiyo huko JKK.
Bi Kyung-Wha Kang amesema, maendeleo na kubuka kwa demokrasia huko JKK itakua vigumu kufanikiwa hadi pale changamoto zilizoelezwa kwenye ripoti hiyo zimechukuliwa kama kipau mbele. Amesema cha muhimu ni kuhamasisha upya juhudi za kukabiliana na suala la kutoadhibiwa wakiukaji. Ripoti inaeleza ni lazima kwa serekali ya Kinshasa kwa msaada wa jumuia ya kimataifa kukabiliana kikamilifu kabisa na wakiukaji na kuhakikisha haitowapa nguvu wanaotaka kutumia nguvu kupata ushawishi wa kisiasa ili kua na udhibiti wa mali asili ya nchi hiyo. Mjumbe maalum wa KM kwa ajili ya watu walopoteza makazi yao IDP's, Walter Kalin amesema hali jumla ya haki za binadam huko JKK inaendelea kua ni ya kutia wasi wasi, na imezorota zaidi tangu kupitishwa azimio la Mrach 2008. Anasema kuna hali mbaya ya kuwahamisha watu kiholela, utumiaji nguvu dhidi ya wanawake na wasichana hasa ubakaji, vitisho na ghasia dhidi ya watetezi wa haki za binadam, mawakili, mahakimu na kuwandikisha kwa nguvu watoto kua wapiganaji.