Skip to main content

Mlinda Amani wa UNAMID auliwa huko Darfur

Mlinda Amani wa UNAMID auliwa huko Darfur

Mlinda amani wa kikosi cha pamoja cha UM na Umoja wa Afrika UNAMID huko Drafur ameuliwa katika shambulio la kushitukiza.

Msemaji wa UNAMID Kemal Saiki amesema, tukiyo hilo halikua ni wizi wa gari wakutumia nguvu bali ni mauwaji ya kikatili tu walikuwa wanawasubiri. Anasema walinda amani walikua wanarudi kutoka kupiga doria wakati watu wanane wakiwa na silaha kuwafyetulia risasi katika mji mkuu wa jimbo la Darfur ya Kusini wa Nyala. Lilikua shambulio la pili tangu mahakama ya kimataifa ICC kumfungulia mashtaka Rais Omar al-Bashir hapo Marchi 4 kwa tuhuma za uhalifu wa vita huko Drafur.