UM unajaribu kuachiliwa huru watumishi wake waliotekwa Somalia

16 Machi 2009

Afisi ya UM ya kuratibu huduma za dharura huko Somalia inasema inatafuta njia za kuachiliwa huru bila ya masharti yeyote wafanyakazi wanne wa afisi hiyo walotekwa nyara Jumatatu asubuhi na washambulkizi wasojulikana.

Taarifa ya ofisi hiyo iliyotolewa huko Nairobi, inaeleza wafanyakazi hao wanne walikua njiani kuelekea uwanja wa ndege wakati mlolongo wa magari yao kusimamishwa na watu walokua na silaha. Hakuna ghasi au ufyetuliaji risasi iliyotokea wakati wa tukiyo hilo huko Waajid, eneo la kati la Somalia. Taarifa inaendelea kueleza kwamba wakati eneo wanaoshikiliwa wafanyakazi hao linafahamika, lakini hakuna mawasiliano yaliyofanyika na watekaji nyara, na kila juhudi zinachukuliwa kuweza kuachiliwa huru bila ya masharti.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter