Ni lazima dunia kusaidia Afrika kunufaika kutokana na juhudi zake za kiuchumi

Ni lazima dunia kusaidia Afrika kunufaika kutokana na juhudi zake za kiuchumi

Naibu katibu mkuu Ashe-Rose Migiro amesema kwamba kwa vile hivi sasa nchi za kiafrika zimefanya mafanikio makubwa katika mageuzi yake ya kiuchumi, inabidi sasa Jumuia ya Kimataifa kuzisaidia kugeuza mafanikio hayo katika kupunguza kwa dhati umaskini.

Akihutubia mkutano mjini Dar es Saalam, Bi MIgiro amesema hivi sasa nchi za Afrika zimeweza kutayarisha mikakati miwili ya kupunguza umaskini hivyo zinahitaji msaada wa kiufundi kuweza kukabiliana na utandawazi na hivyo zinahitaji msaada zaidi. Amesema licha ya maendeleo hayo, hakuna hata nchi moja ya Afrika ambayo iko njiani kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia. Ili kufikia lengo hilo Bi Migiro amasema, msaada zaidi wa kimataifa unahitajika..