Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola milion 50 za Marekani kuimarisha haki za wanawake UNFPA

Dola milion 50 za Marekani kuimarisha haki za wanawake UNFPA

Rais Barack Obama, wa Marekani ametoa dola milioni 50 kusaidia shirika la wakazi la UM UNFPA, ili kupunguza umaskini na kuimarisha afya ya wanawake na watoto katika zaidi ya mataifa 150.

Akitangaza kupokea msaada huo Mkurugenzi Mkuu wa UNFPA, Thoraya Ahmed Obaid, amesema hii ni siku muhimu kwa wanawake na wasichana na familia zao kote duniani, kwani msaada utasaidia kuendelea kuokoa maisha ya watu. Rais Obama, alitia jana sahihi sheria kurudisha tena msaada wa Marekani kwa UNFPA baada ya kusitishwa 2002. Hivyo ametelekeza ahadi aliyotoa alipochukua madaraka kurudisha msaada huo kwa shirika hilo .