Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iran yataka silaha zote za kinyuklia kupigwa marufuku

Iran yataka silaha zote za kinyuklia kupigwa marufuku

Balozi wa Iran, Alireza Moaiyeri amewaambia wajumbe wanaohudhuria Mkutano wa Kupunguza Silaha unaofanyika Geneva, ya kuwa hatua pekee yenye uwezo wa kuuthibitishia, kihakika, umma wa kimataifa usalama dhidi ya vitisho au matumizi ya silaha za kinyuklia ni kwa Nchi Wanachama kuafikiana maafikiano, yanayofungamana na maadili makuu ya kimataifa ya kuondosha, na kuangamiza kikamilifu, silaha zote za kinyuklia, kote ulimwenguni.