Mkariri anayehusika na mauaji nje ya taratibu za kimahakama atazuru Kenya

13 Februari 2009

Philip Alston, Mkariri wa UM juu ya masuala ya mauaji ya kihorera, nje ya taratibu za kimahakama, anatazamiwa kuzuru Kenya kuanzia tareh 16 mpaka 25 Februari, kwa kuitika mwaliko wa Serikali ya Kenya na atakapokuwepo huko atakutana na maofisa wa Serikali kuu na pia zile za majimbo, na vile vile atakutana kwa mashauriano na wabunge.

 Alston anatarajiwa kuwa na mazunguzmo na waathirika wa ukiukaji wa haki za binadamu pamoja na watu walioshuhudia mauaji kufuatia uchaguzi uliofanyika zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Jukumu hasa la Akston kwenye ziara hii linajumlisha ukusanyaji wa ripoti kuhusu madai ya mauaji yaliojiri nchini wakati wa vurugu, na kusailia vyanzo vilivyosababisha kutochukuliwa hatua za kisheria zilizohitajika kuwafikisha mahakamani wale waliohusika na jinai hiyo, ili kukabili haki.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter