Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imefaulu kuwafikia wahamiaji wa JAK wanaohitajia huduma za dharura

UNHCR imefaulu kuwafikia wahamiaji wa JAK wanaohitajia huduma za dharura

Baada ya safari ya siku tatu ya timu ya Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) kwenye eneo la mbali la kusini-mashariki ya Chad, walifanikiwa kuwafikia wahamiaji wa kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, na kuwapatia huduma za kihali, za dharura, kunusuru maisha.

Timu hiyo ya UNHCR pia imeanza kuwasajili wahamiaji karibu 6,000, wingi wao wakiwa watoto wadogo na wanawake wa makabila ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ya Rounga na Sara, ambao walikimbilia Chad kujiepusha na mapigano nchini mwao, yalioanza mwezi Disemba mwaka jana, baina ya makundi ya waasi na vikosi vya Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.