Ofisa wa UNRWA anasema hali Ghaza ni ya kutisha mno
John Ging, Mkurugenzi wa Operesheni za Shirika la UM la Kufarajia Wahamiaji wa KiFalastina kwenye Mashariki ya Karibu (UNRWA) ameiambia Ofisi ya UM, Geneva, hii leo, kwa kutumia njia yasimu, ya kwamba mipangilio ya kuhudumia misaada ya kihali Ghaza, kwa umma muhitaji, imevurugwa kwa sasa, kwa sababu ya kuendelea kwa mapigano, hali ambayo vile vile alisema imeongeza khofu na wasiwasi miongoni mwa wakazi wa Ghaza pamoja na umma wa eneo jirani.