Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yaahidi kuendelea na huduma za kiutu kwa wakazi wa Ghaza licha ya kushambuliwa majengo

UNRWA yaahidi kuendelea na huduma za kiutu kwa wakazi wa Ghaza licha ya kushambuliwa majengo

John Ging, Mkurugenzi wa Operesheni za Shirika la UM Linalofarajia Misaada ya Kiutu kwa Wahamiaji wa KiFalastina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA) aliwaambia waandishi habari mjini Geneva, leo asubuhi, kwa kutumia njia ya simu, ya kuwa licha ya kuwa UM umepoteza misaada ya chakula na madawa iliounguzwa moto baada ya kushambuliwa na makombora ya jeshi la Israel wiki hii, UM hautopwelewa wale kusita kutekeleza majukumu yake ya kuhudumia kihali waathiriwa wa KiFalastina katika Tarafa ya Ghaza.