Takwimu za OCHA zinaashiria wasiwasi wa kupamba kipindupindu Zimbabwe.
Ofisi ya UM kuhusu Misaada ya Dharura (OCHA) imetangaza takwimu zilizothibitisha kwamba jumla ya watu walioambukizwa na ugonjwa wa kipindupindu Zimbabwe ni sawa na wagonjwa 13, 960 na kati ya hao, wagonjwa 589 walishafariki.