Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udhibiti wa kipindupindu Zimbabwe wahatarishwa na ukosefu wa mastakimu safi na maji yanayonyweka.

Udhibiti wa kipindupindu Zimbabwe wahatarishwa na ukosefu wa mastakimu safi na maji yanayonyweka.

Shirika la UM juu ya Mchango wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kwamba mripuko wa maradhi ya kipindupindu Zimbabwe unapaliliwa zaidi kwa sababu ya uchafu – ripoti ilisema waatalaamu wa UM wameshakadiria ya kwamba asilimia 80 ya wananchi Zimbabwe, wamenyimwa uwezo wa kupata maji safi.

“Asilimia themanini ya idadi ya watu nchini, haina uwezo wa kupata maji safi ya kunywa na salama; na wingi wa wazalendo raia, vile vile hawana hata fursa ya kuwa na makazi yalio safi. Kuna uharibifu mkubwa wa vifaa na taratibu zote zinazoambatana na usafi, hasa katika miji mikuu, hali ambayo inatia wasiwasi kwamba bila ya kudhibiti mapema mifumko ya kipindupindu, kuna hatari ya maradhi kusambaa, kwa kasi, katika maeneo makubwa zaidi nchini. UNICEF, hivi sasa, imeanzisha kampeni ya kugonga kila mlango wa makazi ya raia, kwa kulingana na uwezo uliopo wa kifedha na wafanyakazi, ili kuhakikisha familia pamoja na jamii zao huwa wanapatiwa taarifa juu ya nini cha kufanya, kwa wao kujikinga na maambukizo ya kipindupindu, kama kuchukua hatua rahisi, kama zile za kuosha mikono baada ya kwenda haja na kabla ya kula, hatua ambazo inaaminika zikitekelezwa zitasaidia sana katika kunusuru maisha ya watu.”