Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Global Fund imeidhinisha dola bilioni 2.75 dhidi ya UKIMWI, kifua kikuu na malaria

Global Fund imeidhinisha dola bilioni 2.75 dhidi ya UKIMWI, kifua kikuu na malaria

Bodi la Usimamizi wa Taasisi ya Mfuko wa Kimataifa Dhidi ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (the Global Fund) ambalolilikutana New Delhi, Bara Hindi mnamo mwisho wa wiki, limeidhinisha msaada wa fedha wa dola bilioni 2.75, mchango ambao utatumiwa kufadhilia miradi 94 mnamo miaka miwili ijayo, kupambana na maradhi hayo matatu thakili kimataifa.