24 Novemba 2008
Staffan de Mistura, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Iraq, amelaani vikali msururu wa mabomu yalioripuliwa mji wa Baghdad hii leo asubuhi wakati raia walipokuwa wakielekea makazini, mashambulio haya yaliripotiwa kuuwa watu 18 na kujeruhi makumi kadha.