Jumuiya ya kimataifa inahitajia ushirikiano wa pamoja kulinda watumishi wa UM duniani
Ripoti mpya ya KM iliotolewa Ijumatano kuhusu usalama wa wafanyakazi wake ulimwenguni, imetilia mkazo kwamba kunahitajika “ushirikiano wa karibu sana, wa dharura, na uwajibikaji wa pamoja” kati ya UM na Mataifa Wanachama ili kuhakikisha watumishi wa UM, pamoja na wale wafanyakazi wanaohudumia misaada ya kiutu ulimwenguni, hupatiwa hifadhi kinga na usalama kunusuru maisha.