Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM awasilisha Ripoti ya 2008 juu ya Maendeleo ya Milenia

KM awasilisha Ripoti ya 2008 juu ya Maendeleo ya Milenia

Alkhamisi, KM Ban Ki-moon aliwasilisha mbele ya waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu, ripoti nyengine yenye kuelezea juhudi za kimataifa katika kukabiliana na matatizo ya ufukara na hali duni ulimwenguni. Ripoti hii ilikuwa na tathmini kamili kuhusu maendeleo katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) hivi sasa, na miongonimwa mambo iliozingatia ni pamoja na hatua za kimataifa zinazotumiwa kutokomeza umaskini uliotota na kukomesha njaa na masuala yanayohusu usawa wa kijinsia, na taratibu za kupunguza vifo vya watoto wachanga.

Sikiliza taarifa kamili kwenye idhaa ya mtandao.