Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imeripoti wahamiaji 26 kutoka Pembe ya Afrika wamezama Yemen

UNHCR imeripoti wahamiaji 26 kutoka Pembe ya Afrika wamezama Yemen

Mapema wiki hii Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti watu 120 waliokuwa wamesafirishwa kimagendo kutokea Pembe ya Afrika, na kuelekea Yemen, walilazimishwa, kwa kushikiwa bunduki, kuchupa kutoka mashua waliokuwemo katika Ghuba ya Aden, kitendo ambacho kilisababisha watu 26 kati ya umma huo kuzama na kufariki.

Msiba huu umetukia baada ya UNHCR kutoa ripoti yake wiki iliopita iliohadharisha ya kuwa kumeanza kushuhudiwa muongezeko wa watu wabaovushwa kimagendo kutokea mataifa ya Pembe ya Afrika mnamo mwezi Agosti, kwa sababu ya kurejea kwa hali ya hewa shwari katika Ghuba ya Aden.