Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Raisi wa Baraza la Usalama kwa Septemba, Balozi Michel Kafando wa Burkina Faso, kwenye taarifa alioitoa baada ya mashauriano ya faragha juu ya hali katika JKK alieleza wajumbe wa Baraza wana wasiwasi na kuharibika kwa utulivu wa eneo la mashariki katika JKK, baada ya kuzuka mapigano ya karibuni kati ya vikosi vya Serikali (CAF) na kundi la waasi la CNDP. Baraza limesisitiza mapigano hayo yametengua maafikiano ya Goma yajulikanayo kama Actes ‘dEngagement de Goma na kusikitika kwamba walioridhia maafikiano hayo wanaonesha dharau na mapuuza ya ahadi walizotoa hapo kabla. Baraza limewataka wafuasi wa CNDP kukomesha haraka operesheni zao na linazingatia pia taarifa iliotolewa na kundi hilo ya kuahidi kuondosha vikosi vyao halan kutoka kwenye jukwaa la mapigano.

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navanethem Pillay alipohutubia Baraza la Haki za Binadamu Ijumaa kwenye mjadala wa mwaka juu ya suala la usawa wa kijinsia alihimiza nchi wanachama kutumia juhudi zote kufuta sheria na mila zinazokandamiza mafanikio yaliopataikana katika kuwasilisha usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake. Alisema tngu Azimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu lilipoidhinishwa kulipatikana maendeleo makubwaya kutia moyo katika utekelzaji wa sheria za kitaifa, sera na miradi inayohusu madaraka ya kuwapatia wanawake fursa ya kushiriki kwenye maendeleo ya kiuchumi na jamii. Alisisitiza bado hatua kubwa zinatakiwa kuchukuliwa na jamii ya kimataifa kuhakikisha usawa kamili wa kijinsia unatekelezwa kwa natija za wote kote duniani.