Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo vya watoto wachanga vinateremka duniani, UNICEF inasisitiza

Vifo vya watoto wachanga vinateremka duniani, UNICEF inasisitiza

UNICEF imewasilisha ripoti mpya wiki hii yenye yenye takwimu zenye kuonyesha maendeleo kwenye juhudi za kimataifa katika kupunguza vifo vya watoto wachanga kwenye mataifa yanayoendelea, kwa kulingana na lengo la nne la Malengo ya Mandeleo ya Milenia (MDGs). Miranda Elles, Msemaji wa UNICEF aliwaambia waandishi habari Geneva kwamba katika 2007 utafiti wa UM umethibitisha kuteremka kwa kima cha kutia moyo kwa vifo vya watoto wachanga duniani.